Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mkutano Wa CHADEMA Mbuguni, Machi 20 Katika Picha

DSCN0138Mamia ya wananchi wa Kijiji cha Mikungani, Kata ya Mbuguni wakisikiliza kwa makini sera zikinadiwa na Dr Slaa kwa ajili ya kumuombea kura mgombea wa uchaguzi jimbo la Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nassari

DSCN0165Dr Slaa akisisitiza jambo mkutanoni hapo….

DSCN0172Mgombea Ubunge Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nassari akfuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wake wakati akisubiri zamu yake kuzungumza…

DSCN0153Huyu aliamua kutoka kwa style hii..

DSCN0158Pamoja na kwamba hakuna usafiri wa daladala kama mijini, bado wananchi hawa waliweza kutembea umbali mrefu kutoka kona tofauti za kata ya Mbuguni ili kuweza kusikiliza kile CHADEMA walipanga kuwaambia

DSCN0178Wilfred Lwakatare, akitaka ufafanuzi toka kwa maofisa wa Polisi juu ya matukio ya kuhujumu kamapeni za CHADEMA yanayohusishwa na CCM kama mhusika mkuu

DSCN0149Mchungaji Natse alikuwepo uwanjani

DSCN0130Kina mama ambao hawakwenda mkutanoni, waliweza kuonesha hisia zao pindi msafara wa viongozi na wafuasi wa CHADEMA ulivyokuwa unaondoka Mbuguni

DSCN0179Mdau wa Blog hii akiwa amepozi na maofisa wa CHADEMA. Kutoka Kushoto Bruno Kimaryo, na Anande Nkya

DSCN0115Mzee huyu na Mkewe walishindwa kuzuia hisia zao mara baada y kuona bendera ya CHADEMA inapepea garini

DSCN0189Kina mama na wababa nao hawakukisekana..        

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO