Taarifa za ndani kutoka CHADEMA zinaeleza kuwa chama hicho kimeandaa hafla ya chakula cha jioni, Ijumaa ya Machi 16 itakayowajumuisha viongozi, marafiki, wapenzi na wanachama wa CHADEMA mjini Arusha na maeneo ya jirani.
Halfla hiyo inayotarajiwa kufanyika katika Hotel ya Naura Spring kuanzia majira ya saa 12 za jioni, imeandaliwa maalumu kwa ajili ya kukusanya fedha za kugharamia kampeni za chama hicho Jimboni Arumeru Mashariki.
Jumla ya watu 500 wanatarajiwa kujumuika kwa chakula cha pamoja jioni hiyo kwa hafla ya kuchangia chama ambayo inatarjiwa kurushwa mojakwamoja na vyombo vya habari.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba alisema nia ya chama hicho kukusanya fedha kupitia mikutano ya kampeni na hafla kama hii ni kutaka watu wajione ni sehemu ya CHaADEMA katika shughuli mbalimbali za chama.
Mwigamba anasema viongozi wengi wa chama hicho watahudhuria hafla hiyo wakiwemo Mwenyekiti wa chama taifa MhFreeman Mbowe, na Katibu Mkuu wake Dr Wilbroad Peter Slaa ambae alikuwa nje ya nchi na hivyo kukosa sherehe za ufunguzi wa kampeni za chama chake. Pia wabunge wake machachari, madiwani na viongozi wa chama hicho toka mikoa ya jirani waanatarajiwa kuhudhuria.
Machi 10, siku ya ufunguzi wa kampeni zake katika uwanja wa Shule ya Msingi Leganga, Usa-River, Arumeru, CHADEMA ilizindua rasmi mpango huu wa watu kukichangia chama kiasi chochote kile kata kama ni shilingi mia, na kufanikiwa kukusanya jumla ya Sh milioni 8 kutokana na harambee ya kukichangia ikwa ajili ya kampeni jimboni humo.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba alisema fedha hizo zimekusanywa kupitia michango ya papo kwa papo na simu. Alisema Sh2.2milioni zilikusanywa uwanjani na Sh5.7 milioni zilikusanywa kwa njia ya simu hadi kufikia Machi 11 jioni.
Tangu kuzinduliwa kwa mpango huu mpya wa CHADEMA kuwashirikisha wananchi moja kwa moja kwa kuchangia kiasi chochote ili wajione kama sehemu ya mafanikio ya chama, utaratibu huo umekuwa ukifanyika katika mikutano yote waliyofanya hadi sasa katika maeneo tofauti Jimboni humo, na wananchi wamekuwa na mwamko mkubwa kushiriki uchangiaji huo.
Katika hatua nyingine, Meneja wa Kampeni za CCM Jimboni humo, ambae pia ni Katibu wa Uchumi na Fedha wa chama hicho, akihutubia mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama chake, aliwapiga vijembe CHADEMA na kujeli mpango wao huo wa kuchangisha hela kwenye kampeni akidai ni kuwakejeli wananchi kuwachangisha sh 50 wakati wanatumia helcopta ambayo inagahrimu Sh 2.5 milioni kwa saa.
Katika hali ambayo inatafsiriwa ni kujibu mapigo, Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akihutubia katika mkutano wa kumnadi mgombea wa chama chake katika viwanja vya Chuo Cha Ualimu Patandi, Tengeru juzi, alisema Mwigulu Nchemba anatoka katika moja ya majimbo masikini zaidi nchini mahali ambako wananchi wanavaa kandambili za rangi tofauti lakini ni ajambu anazunguka na maburungutu ya hela na kugawia watu.
Lema alienda mbali zaidi na kuhoji kama kweli Mwigulu anafikiria kuwasaidia watu kwa kuwagawia hela, kwanini hizo fedha anazogawa asingezitumia kuondoa umasikini na kero za watu wake huko Singida?
0 maoni:
Post a Comment