Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Jeshi la Polisi Limewafukuza Kazi Askari Wake Wanne Waliompiga Mwananchi wa Urambo Tabora Hadi Kufa

Jeshi la Polisi limetangaza kuwafukuza kazi na kuwafikisha mahakamani askari wake wanne waliokuwa wanashikiliwa Wilayani Urambo kwa tuhuma za kumshushia kipigo mwananchi mkazi wa mjini Urambo hadi kusababisha kifo chake.

Akitoa maelezo hayo jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora S.S.P Yusuf Mruma ameeleza kuwa hizo hatua za mwanzo za Jeshi la Polisi kukabiliana na vitendo vilivyo kinyume cha sheria na kwamba askari hao watafikishwa mahakamani kesho (leo) kusomewa mashataka yanayowakabili.

Mwananchi huyo Hassan Mgalula, ameelezwa kupigwa hadi kufa na askari wenye namba G 3037 Pc Aidano, namba G 3836 Pc Jonathan, namba G 4836 Pc Mohamed, na namba G 5382 Pc Khakimu.

Aidha, Diwani wa kata ya Urambo Mjini, Amatus Ilumba,amesema chanzo cha kipigo kwa kijana huyo ni ugomvi uliotokea baina yake na askari mmojawao takribani wiki mbili zilizopita na Jumatano walipokutana polisi na huyo aliwaita wenzake na kuanza kumpiga na baadaye kusababisha kifo chake.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,aksari polisi hao walimpiga Mgalula pasipo kujali hadi kumfanya awe hoi huku akijisaidia haja ndogo na kubwa pasipo kupenda. Mashuhuda hao walizidi kueleza kuwa Mgalula alifariki hata kabla hajafikishwa Hospitalini kutokana na hali yake aliyokuwa nayo huku wakiongeza kuwa hata Polisi wenyewe walijua kuwa tayari alikuwa amekwisha fariki.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira walikuwa na mpango wa kukivamia kituo cha Polisi Urambo ili kuhakikisha kuwa kama kweli uongozi wa juu wa jeshi hilo ngazi ya mkoa umechukua hatua ya kuwashikilia askari hao ili baadaye sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Bi Anna Magova aliwasihi wakazi wa Urambo kuwa watulivu na kuwataka kuvipa ushirikiano vyombo husika katika kushughulikia swala hilo!

Chanzo: TBC1 na KAPIPI Jhabari.COM

N.O.I.S.E.O.F.S.I.L.E.N.C.E BLOGA KEEPS U UPDATED
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO