Magari ya Maji ya Kuwasha Yawasili Arusha
Katika kile kinachoonekana kuwa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linajiimarisha kiulinzi katika kujiweka tayari kukabiliana na vurugu zozote zinazowezakujitokeza katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, magari ya kumwaga maji ya kuwasha yamewasili mjini hapa.
Uchaguzi wa Arumeru Mashariki unatarajiwa kufanyika Aprili Mosi na kampeni za wagombea zinatarajiwa kufunguliwa rasmi mwishoni mwa wiki hii!
Baadhi yamashuhuda wameeleza kuona magari hayo yakisindikizwa kwa ulinzi mkali kuelekea maeneo ya Arumeu na kuhoji uhalali wa kuwa na vifaa kama hivyo na kuimarisha ulinzi kiasi hicho kwa mahali na watu wenye utulivu. Pengine hii ikwa imechangiwa na historia ya ushindani mkubwa wa kisiasa ulipo baina ya wafuasi wa vyama viwili vinavyopewa nafasi kubwa ya kimoja wapo kuibuka mshindi katika uchaguzi huo!
N.O.I.S.E.O.F.S.I.L.E.N.C.E KEEPS U UPDATED
0 maoni:
Post a Comment