Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kesi ya Kupinga Ushindi wa Lema: Dr Batilda Ashindwa Kutokea Mahakamani Kutoa Ushahidi


Wananchama wa CCM waliofungua shauri kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita Jimbo la Arusha Mjini, wamejikuta wakiondoka mahakamani vichwa chini baada ya shahidi waliyemtegemea kushindwa kutokea kwa ajili ya kutoa ushahidi katika kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, katika kesi inayosikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Shahidi huyo, Dr Batilda Buriani ameondolewa katika orodha ya mashahidi kwa upande wa walalamikaji na ushahidi kwa upande wao umefungwa. Kati ya mashahidi 25 waliotarajiwa kutoa ushahidi kwa upande wa walalamikaji ni mashahihi 14 tu ndio wameweza kujitokeza.

Wakili wa walalamikaji, Bw Alute Mughwai alisema kuwa Dr Batilda Buriani ameondolewa kwenye orodha ya mashahidi katika shauri husika kutokana na kutingwa na majukumu mengine ikiwemo kuwasilisha nyaraka za utambulisho wake kama Balozi wa Tanzania Kenya, nafasi aliyoteuliwa na Rais Kikwete hivi karibuni.

“Tulitaraji kuwa Dr Buriani angwasili mjini Arusha Jumamosi iliyopita ili kuweza kutoa ushahidi wake Jumatatu lakini haikuwa hivyo. Baada ya kupitia ushahidi uliokwisha tolewana ma mashahidi 14 mpaka sasa, tumeamua kutomuita tena kwasababu tumeshapata tulichokuwa tunahitaji katika ushahidi" alikaririwa Bw Mughwai.

Bw Mughwai alieleza hayo akijibu swali la Mwendesha Mashitaka Jaji Gabriel Rwekibarila alietaka kujua kwanini Dr Buriani hakuitwa kutoa ushahidi wake ilihali alikuwa mgombea katika Uchaguzi Mkuu uliopita kwa tiketi ya CCM, ambao mshindi wake anapingwa Mahakamani hapo, na ni shahidi muhimu kwasababu jina lake limetajwa na mashahidi wengine wote 14.

“Huyu ni shahidi muhimu sana katika shauri hili kwakuwa jina lake limeteajwa na kila mmoja wa mahshidi 14 waliotoa ushahidi wao. Nina uhakika yeye ndie msingi wa shauri hili kwa tuhuma zilizotolewa dhidi yake (wakati wa kampeni. Kwanini usimuite ili kuisaidia Mahakama? alihoji mwendesha shauri, ane wakili wa walalamikaji akajitetea kwa kusema kwamba hawana dhamria ya kumuita Dr Buriani na kama Mahakama inaona ni muhimu yeye kutoa ushahidi wake, basi inaweza kumtumia kama srafiki wa Mahakama.

Hata hivyo, Jaji Rwakibarila alipinga na kudai kuwa sio jukumu la Mhakama kufanya hivyo na kumpa muda Wakili wa walalamikaji muda zaidi ili Br Buriani amalize shughuli zake za kibalozi na aweze kutokea kutoa ushahidi lakini Wakili akasisitiza kuwa hawahitaji tena Dr Buriani atoe ushahidi wake.

Akiongezea, Bw. Mughwai akasema kuwa hawatamuita tena shahidi wa 15 alieshindwa kutoa ushahidi siku ya Ijumaa baada ya kujisjiskia kuumwa kabla ya kutoa ushahidi wake. Kufuatia hali hiyo, Wakili wa Utetezi, Mr Method Kimomogoro aliemwakilisha Mh Lema, aliiomba Mahakama kuwapatia siku mbili hadi Ijumaa ili kuandaa ushahidi kwa upande wa utetezi.

Wiki ijayo Mahakama itakuwa ikisikiliza mashahidi wa upande wa utetezi, na Lema anategemewa kutoa utetezi wake Ijumaa hii.
Read more...
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO