Chanzo: Happy Lazaro, Mwananchi
MGOGORO kati ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) na Wasafirishaji Abiria kwa kutumia gari aina ya Noah Mkoa wa Arusha umeshika kasi baada ya wafanyabiashara hao kuitaka Serikali kuzuia Mamlaka hiyo kusitisha biashara ya gari hizo kwani hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo.
Kufuatia agizo hilo la Sumatra, Umoja wa Wasafirishaji Abiria Arusha kwenda Namanga (Nasa) umewaandikia viongozi wa Mkoa wa Arusha ambao ni Mkuu wa Mkoa, Wabunge wa Monduli, Longido, Karatu, Arusha mjini, Mkurugenzi Mkuu Sumatra na Mkuu wa Usalama Barabarani wakipinga agizo hilo na kutishia kuhamasisha maandamano nchi nzima.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao juzi jijini hapa, walidai iwapo agizo hilo litatekelezwa wakati huu ambao mamilioni ya Watanzania wanasaka ajira kila kukicha, maelfu ya ajira za madereva wa gari hizo zitapotea na kupunguza mamilioni ya fedha zinazokusanywa na Serikali kupitia kodi na ushuru unaotokana na biashara hiyo. Gonga hapa kujua agizo la SUMATRA kusitisha leseni za magari aina ya Noah kubeba abiria nchi nzima ifikapo Juni 31, 2012.
Soma zaidi habari hii...
Home
Uncategories
Umoja wa Wasafirishaji Abiria Arusha kwenda Namanga (Nasa) Wapinga Agizo la SUMATRA Kusitisha Leseni Ifikapo Mwezi Juni
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment