Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka. Kwa kawaida matukio mengi hufanyika ikiwa ni ishara ya kuienzi siku hiyo muhimu katika historia ya mwanamke.
Katika kuweka msisitizo wa siku hiyo maalum, wanawake wengi wameutambua mwezi Machi kama mwezi wa mwanamke kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kisiasa na kiuchumu zinazolenga kuonesha mchango wa mwanamke katika jamii.
Mkoani Arusha kumekuwepo na maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazozalishwa na mwanamke ama zinamhusu mwanamke kwa matumizi, ama uhitaji wake katika majukumu yake ya kila siku katika jamii yake. Maonesho hayo yanafanyika katika bustani za Jiji jirani na Impala Hotel, mzunguko wa Kijenge.
Bidhaa mbali mbali na huduma za ushauri zimekuwa zikitiolewa kw wageni wanaozuru mabanda tofauti tangu kuanza kwa maonesho hayo, Machi 1 yakitarajiwa kufikia tamamti siku ya kilele Machi 8 ya mwaka huu.
Watu wengi wameonekana wakivutiwa zaidi kutembelea mabanda yaa Perteners for Development na Tanzania Domestic Biogas Program (TDBP) kwasababu ya teknolojia mpya walizokuwa wanazionesha katika kumsaidia mwanamke kiuchumi na kijamii. Banda la Partners for Development wanaonesha ubunifu wao katika JIKO BOMBA Rafiki wa mapishi na mazingira.
TDBP wameleta katika maonesho haya ubunifu wa mtambo wa kuzalisha Biogas kwa ajili ya matumizi mbalimabali na hivyo kumpunguzia mwamanke gharama fulani.
Mchoro ukionesha mfumo mzima wa uzalishaji Biogas
Mfano wa mashine iliyobuniwa kutumia nishati ya jua kwa ajili ya kuchemshia maji (kushoto) na kukaushia nafaka ama mboga (kulia)
N.O.I.S.E.O.F.S.I.L.E.N.C.E BLOGA KEEPS U UPDATED
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment