Mvurugano mkubwa unaendelea muda huu katika ofisi za Manispaa Ilala ambapo walimu waliopata ajira hivi karibuni wamevamia ofisi hizo wakidai mishahara yao!
Itakumbukwa kuwa jumla ya walimu 23,907 wa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu walipata ajiria Serikalini katika mwaka wa fedha 2011/2012. Miongoni mwao ndio hao waliojikusanya katika ofisi hizo kujua hatma ya mishahara yao.
Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa hii, walimu hao tayari wameshaonana na Afisa Utumishi wa Manispaa na kuwaeleza kuwa mishahara yao haitaweza kupatikana kwa mwezi huu kwasababu kulikuwa na matatizo ya kiufundi yaliyosababisha kushindikana kuscan majina ya walimu hao na kuyatuma hazina kwa uandaaji orodha ya malipo katika muda muafaka.
Kana kwamba walimu hao hawakuridhishwa na majibu hayo ya afisa huyo, wanazidi kuhoji iweje wenzao wa Mwanza, Mara, Singida na mikoa mingine wapate mishahara yao kwa wakati halafu wao wa Dar wakose?
Hadi mtoa taarifa anaondoka eneo la tukio mchana huu, bado walimu whao wameendelea kuwepo wakimsubiri Mkurugenzi wa Manispaa ili kuweza kupata ufumbuzi wa swala lao.
Gonga hapa kuona orodha kamili ya ajira mpya za walimu katika mwaka wa fedha 2011/2012.
N.O.I.S.E.O.F.S.I.L.E.N.C.E
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment