Lula Wa Ndali Mwananzela anaandika....
SIJUI Spika wa Bunge, Anne Makinda anawafikiriaje Watanzania. Vyovyote vile, kauli zake za siku chache zilizopita zinatudokeza tu kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba, Spika Makinda anawachukulia Watanzania kama watu wasioweza kufikiria, wasiojua kutofautisha ukweli na uongo na ambao wanaweza kuzugwa kiurahisi kwa maneno yanayotolewa na wale ambao wana bendera zenye kupepea kwenye kona za magari yao.
Kwa mara nyingine tena – na pasipo sababu ya msingi – Spika Makinda amejaribu kuhalalisha tena ongezeko kubwa la posho za wabunge kiasi cha kutudokeza kuwa ni shilingi 200,000 kwa siku tisa na kuwa “kuna vikao vinne kwa mwaka na ni vitatu tu ambavyo wabunge watalipwa” kiasi hicho. Kwa maneno mengine wabunge wapatao 357 watalipwa shilingi 71.4 milioni kwa siku na kwa siku hizo tisa walipwe shilingi 642.6 milioni!
Spika Makinda anatuambia tusilalamike kwa kuwa kwa vikao vile vitatu vya siku tisa tisa hawa wabunge wetu maskini walipwe shilingi bilioni 1.9 hivi. Hizi ni posho tu!
Yaani hawa wabunge wetu ambao watalipwa posho hizo bado watalipwa mshahara usiopungua shilingi milioni 2.5 kwa mwezi ambayo ni sawa na milioni 892.5 kwa mwezi kwa wabunge wote, au sawa na bilioni 10.7 kwa mwaka. Hapa tunazungumzia mshahara tu na posho.
Hapa hatujaingiza posho nyingine lukuki na mapato mengine wanayoyapata wanapohudhuria semina, mikutano na vikao vingine ambavyo wanalipwa kwa kiwango kile kile cha per diems za kibunge!
Makinda anataka tuamini kuwa hawa ni maskini! Soma zaidi uchambuzi wa LULA WA NDALI MWANANNZELA, Raia Mwema
N.O.I.S.E.O.F.S.I.L.E.N.C.E
Home
Uncategories
Makala: Kati ya Viongozi ambao Hawana uwezo wala Nafasi ya kuzungumzia Umaskini ni Anne Makinda.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
1 maoni:
Kiukweli kabisa Spika Makinda ameshindwa kujua dhamana aliyonayo kwa mustakabali wa taifa kwa kusimia Mhimili muhimu sana katika uongozi na ustawi wa nchi...
Amepwaya kwenye hiyo nafasi
Post a Comment