Ujenzi wa mradi mkubwa wa bandari na utakaogharimu $23bilioni (£14.5bn) kusini mashariki mwa pwani yaKenyakatika mji wa Lamu karibu na mpaka wa Somalia umezinduliwa.
Bomba la mafuta, reli na barabara pia zitajengwa kuunganisha Lamu na Sudan Kusini na Ethiopia.
Nchi iliyopata uhuru wake hivi karibuni ya Sudan Kusini ina mipango ya kutumia Lamu kama njia kuu ya kusafirishia mafuta yake.
Mwandishi wa BBC anasema wasiwasi kuhusu usalama wa mradi huo unaweza kuelezea umuhimu wa kuwepo kwa vikosi vya Ethiopia na Kenyan chini Somalia vikilenga kulipatia utulivu eneo hilo.
Rais wa Kenya Mwai Kibaki alizindua mradi huo sambamba na Rais wa Sudan Kusini na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi.
"Sina mashaka kuwa siku hii itakumbukwa katika historia wakati tunapojaribu kuwaunganisha watu wetu na kupata fursa za muhimu za kiuchumi na kijamii kwa ajili ya maishayaoyajayo" Shirika la habari la AFP limemnukuu Rais Kibaki akisema wakati wa sherehe za uzinduzi.
Ikifahamika kama kama Bandari ya Lamu ya usafiri ukanda wa Sudan Kusini Ethiopia(Lapsset), inatarajiwa kumalizika kwa miaka minne ikiwa na gharama za awali kutoka serikali hizo tatu huku mipango ya kuwaalika wawekezaji wa kimataifa ikiwekwa.
Kwa maelezo zaidi ungana na BBC Swahili
N.O.I.S.E.O.F.S.I.L.E.N.C.E KEEPS U UPDATED
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment