Diwani wa CCM, Thomas Mollel ‘Askofu’ akamatwa na (TAKUKURU) kwa kutoa rushwa kwa madiwani Arumeru.
GAZETI HabariLeo linaripoti kuwa, wakati mwanachama wa CCM, Siyoi Sumari, akitangazwa mshindi katika mzunguko wa pili wa kura ya maoni Arumeru Mashariki, mfanyabiashara maarufu mkoani hapa anayechimba, kuuza na kununua madini aina ya tanzanite, Thomas Mollel ‘Askofu’ amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa madiwani.
Askofu huyo ambaye pia ni Diwani wa Mbuguni, Arumeru, alikamatwa usiku wa manane wa kuamkia jana kwa tuhuma hizo zinazohusiana na kura ya maoni ambayo ilipigwa jana na kumpa Siyoi ushindi wa kura 761 dhidi ya William Sarakikya ambaye alipata kura 361.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, iliagiza kurudiwa kwa kura ya maoni ikihusisha wagombea hao baada yao na wengine waliojitokeza kutofikisha zaidi ya nusu ya kura za wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Katika kura hizo, Siyoi aliongoza kwa kupata kura 361 akifuatiwa na Sarakikya aliyepata kura 259. Kamati Kuu ilifanya uamuzi huo ili kupata mgombea ambaye atapata asilimia 50 au zaidi ya hapo.
Soma zaidi...
0 maoni:
Post a Comment