Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mandhari Mwanana Katikati Ya Mji Wa Arusha

Kwa mtu ambae aliondoka Arusha miezi kadhaa iliyopita, akirudi na kutembelea barabara ya Boma/Makongoro, atajionea mabadiliko makubwa katika muonekano wa eneo lililoachwa kwa muda mrefu bila kupambwa na kuishia kuwa danguro la machangudoa kipindi cha nyuma!

Uwekezaji uliofanywa na wamiliki wa hoteli mpaya ya Palace Hotel Arusha, ambayo nayo inatazamana na bustani hii, umeweza kuweka mandhari nzuri na kutoa nafasi kwa watu kupata nafasi ya kupumzika kwenye viti maridadi huku wakifurahia upepo wa Geneva ya Africa.

Kama picha inavyoonesha, eneo hili limetengenezwa vizuri hadi kuwa kivutio kwa wageni wengi, na hata wenyeji.

Kwa kawaida miji yetu huwa kuna tatizo la mamlaka kutoacha ameneo wazi kwa mapumziko ya raia na kuwa mahali pa mji kupumulia.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO