Chanzo BBC
Uchumi mkubwa barani Afrika unatarajiwa kuathirika kufuatia maandamano makubwa yatakayoshirikisha mamiya ya wanachama wa mashirika ya wafanyakazi kote nchini Afrika ya kusini, wakipinga kuanzishwa kwa kodi ya barabara pamoja na mpango wa ajira kupitia mikataba ya mda mfupi.
Vyama vya wafanyakazi vya Afrika ya kusini vimekua na migongano na mpango wa serikali wa vituo vinavyotumia mitambo ya electroniki kukusanya pesa kutoka kwa watumiaji wa barabara.
Shirika la Cosatu lilitarajia kua maandamano hayo yatahudhuriwa na maelfu ya watu kupinga mfumo huu mpya pamoja na mawakala wa ajira. Maandamano hayo pia yanalenga kuondoa tabia ya kupanga ajira ambapo mashirika huajiri watu kwa mkataba wa mda mfupi.
Maandamano hayo yaliyoandaliwa na Chama cha wafanyakazi COSATU, ilipangwa kufanyika katika miji 32 kote Afrika kusini.
Soma zaidi..
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment