Lowassa Yuko Hospitalini
Jana, Lowassa akizungumza na mwandishi wa Mwananchi kwa simu alisema kwamba yuko hospitali, bila kufafanua kuwa ni nje au ndani ya nchi, wala kueleza kinachomsibu.
Mahojiano hayo kati ya Lowassa na mwandishi yalikuwa kama ifuatavyo:
Swali: Asalaam alaykum Mheshimiwa Lowassa.
Jibu: Waalaykum Salaam.
Swali: Mimi naitwa... (jina la mwandishi) kutoka gazeti la Mwananchi. Kwanza pole kwa matatizo ya kiafya yanayokusumbua.
Jibu: Ahsante.
Swali: Nimekupigia pamoja na kukupa pole, nilitaka kujua unaendeleaje na matibabu?
Jibu: Niko hospitalini kwa sasa naomba niache mambo mengine tutaongea baadaye.
Swali: Lakini, ni matibabu gani hasa unayopata?
Jibu: ... (akimtaja mwandishi) naomba niache niko hospitalini sasa hivi mambo mengine tuongee baadaye.
Lowassa alitoa majibu hayo majira ya saa nane mchana na alipopigiwa tena saa 10.20 jioni, alijibu kama ifuatavyo:
Swali: Naam, Mheshimiwa Lowassa nimekupigia tena mimi... (mwandishi akajitambulisha).
Jibu: ... Unataka nikuambie nini tena? Nilishakwambia niko hospitalini niache!
Swali: Sawa, natambua uko hospitalini, lakini wewe ni kiongozi ambaye umewahi kuwa Waziri Mkuu, hivyo Watanzania wangependa kujua maendeleo ya afya yako kutokana na utata ulioibuka na kama je, umelazwa hapo hospitalini au uko katika matibabu ya kawaida?
Jibu Niache, ninachokwambia niko hospitalini sasa unataka nini tena? Nisingependa kuzungumzia afya yangu kwa undani.
Soma zaidi...
0 maoni:
Post a Comment