Wagombea 8 Kuchuana Arumeru Mashariki
Jumla ya vyama 8 vimejitokeza kushiriki uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki unaotarajiwa kufanyika April mosi mwaka huu ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi baada ya kufariki kwa aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo marehemu Jeremia Sumari.
Akitangaza majina ya wagombea leo ikiwa ni siku ya mwisho kurudisha fomu, Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Trasias Kagenzi ametaja washiriki hao na vyama vyao kwenye mabano kuwa ni Joshua Nassari (Chadema), Abrahamu Chipaka (TLP), Mohamedy A. Mohamedy (DP), Charles Msuya (UPDP), na Sioi Sumari (CCM)
Wengine ni Hamis Juma Kiremi (NRA),Abdala Juma Mazengo (AFP) na Shabani Kirita Moyo (SAU)
Kagenzi alisema jumla ya wapiga kura wasiopungua 127,000 wa tarafa tatu za jimbo hilo lenye kata 17 wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo.
Msimamizi huyo wa uchaguzi127,000 wa tarafa tatu za jimbo hilo lenye kata 17 zinapaswa kuwa na wadhamini wasiopungua 25 na wasizidi 31 na wawe wapigakura ambao waliandikwa kwenye daftari la kupigia kura.
Msimamizi huyo alisema kuwa hakuna pingamizi lolote lilopokelewa hadi sana na wagombea wote wameweza kukidhi mahitaji kisheria, kinachosubiriwa ni pingamizi endapo litajitokeza na mwisho wa kupokea pingamizi kwa wagombea itakuwa kesho saa 10 jioni.
Kwa utaratibu uliotangazwa mapema wiki hii, ilielezwa kuwa kila mgombea anapaswa kuwa na wadhamini wasiopungua 25 na wasiozidi 31 ambao wapo kwenye orodha ya wapiga kura.
Hata hivyo, pamoja na wingi huo wa washiriki katika uchaguzi huu, wachambuzi wa mambo ya kisiasa hususani kwa hali ya Arumeru Mashariki, mchuano utakuwa mkali baina ya wagombeA WA CHADEMA na CCM. Mgombea wa CHADEMA anaingia akiwa na rekodi nzuri kwa uchaguzi uliopita ambapo mzazi wa mgombea wa CCM aliibuka mshindi. Mgombea wa CCM anaingia kwenye uchaguzi huu akiwa hana historia katika siasa za nchi hii zaidi ya historia ya mzazi wake amabe ni marehemu kwa sasa.
0 maoni:
Post a Comment