Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Jikumbushe Kauli Tofauti Za Waziri Mkuu Pinda Kuhusu Mgogoro Wa Madaktari Nchini


WAKATI madaktari wakisisitiza kufanya mgomo waliouita wa kihistoria kuanzia leo kushinikiza kuondolewa madarakani kwa Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewasihi wataalamu hao wa afya kutochukua hatua hiyo kama kweli wana nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Waziri mkuu Pinda alisema Serikali haioni sababu ya kuwawajibisha mawaziri hao kwa sasa na kueleza kushangazwa kwake na hatua ya madaktari hao kugeuza suala hilo kuwa dai namba moja hivi sasa.

Akizungumza kwa tafsiri ambayo wengi wanaona ni kama kumtetea Dr Mponda, Pinda alisema Dk Mponda mwenyewe anayelalamikiwa ndiyo kwanza ana mwaka mmoja na nusu kazini na hata madai mengine hayajui kwa kuwa hakuwepo wakati huo akisema shinikizo la kutaka awajibishwe ni kumuonea.

Baadhi ya wanachi waliotoa maoni yao kuhusu sakata hili wamesikitishwa na hali inavyoendelea bila kuwa na dalili za kupatikana muafaka

HEBU TUJIKUMBUSHE KAULI KADHAA ZA WAZIRI MKUU KUHUSU KADHIA HII YA MGOGORO WA MADAKTARI NA SERIKALI

Janur1 29, 2012; Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam
"..Daktari atakayegoma kesho atakuwa amejifukuzisha kazi. Na mikutano yao (madakatari) ni marufuku kufanyika popote pale.."

Februar1 9, 2012; Hospitali ya Rufaa Muhimbili, Dar es Salaam.
"Nimeamua kuwasimamisha kazi Mganga Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Waizara ya Afya, ili kuweza kupisha uchunguzi maana hizi tuhuma zinafedhehesha taifa. Kwa upande wa Waziri na naibu wake nimeshapeleka ushauri kwa Rais kutokana na yeye kuwa mwenye dhamana, siwezi kuliongelea hili hapa ila yule aliewateua atafanya maamuzi, najua kitakachofuata mtakijua.."

Machi 6, 2012; Ofisini Kwake-Dar es Salaam
“Hivi kweli mnataka nifike mahali nimwaambie Rais tunakupa saa 72 uwafukuze kazi viongozi hao? Hapana... hapana... hapana kwa lipi hasa? Siwezi kumwambia atekeleze hayo. Ingekuwa hatujafanya chochote sawa, hata angekuwa mtu yeyote hawezi kukubalina na hayo unless (vinginevyo) wenzetu madaktari watuambie wana hoja nyingine.”

Machi 6 hiyo hiyo, alipoulizwa endapo mawaziri hao wataamua kuwajibika wenyewe ili kunusuru maisha ya Watanzania, Serikali yake itakuwa tayari kwa hilo? Akahoji: “Kwa lipi hasa? Naona ni vyema tusubiri majadiliano, hayo yote yatajulikana baada ya kufikia mwisho.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO