Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Wananchi Arusha Waandamana Kwa Mkuu Wa Mkoa Kudai Ardhi Yao Iliyoporwa Na JWTZ


Mji wa Arusha uliingiwa na taharuki kwa muda na kuibua hofu kwa baadhi ya watu baada ya kushuhudia mamia ya watu wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo hii majira ya saa & mchana.

Hii ni kufuatia wananchi kutoka kata tatu za Mlangalini, Moshono na Nduruma wilayani Arumeru mkoani Arusha, wameandamana hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, wakipinga kitendo cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 977 KJ kuwanyang’anya ardhi yao.

Wakazi hao ambao walianza safari hiyo kutoka Mushono na kukumbwa na vikwazo vya Polisi waliokuwa wakiwazuia wasiendelee na maandamano hayo, lakini ilishindikana.

Katika maandamnano hayo, walikuwa wakiimba nyimbo za kuhamasishana huku wakipeperusha matawi ya miti hadi ilipo ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kushinikiza kupatiwa majibu ya mgogoro wa ardhi baina yao na Jeshi la wananchi unaodaiwa kudumu kwa takriban miaka mitatu sasa. Na wakadai kwa muda wote huo Serikali imeshindwa kumaliza mgogoro huo na huku Jeshi likiwazuia kufanya maendeleo yoyote katika ardhi yao.

Wakazi hao, mchanganyiko wa wazee, vijana hadi watoto, wamama, wadada, wakaka kwa wanaume baada ya kutembea kwa zaidi ya km 10, walijikuta wakiishia nje ya uzio baada ya mageti kufungwa mapema kabla hawajafika.

Hata hivyo uongozi wa mkoa uliweza kujitokeza na kuzungumza naoan hatua iliyosaidia kutuliza munkari ya wananchi hao walioonekana kuwa na hasira. Mkuu wa Mkoa alizungumza nao kwa utulivu sambamba na mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wengine, na kuafikiana na wananchi hao kwamba ifikapo tarehe 23 Machi,2012 majibu rasmi ya mgogoro husika yatakuwa yamepatikana.

Baadhi ya wananchi hao walisikika wakiahidi kujitokeza kwa wingi zaidi siku hiyo waliyokubaliana kupatiwa ufumbuzi wa mgogoro huo.

Wakati huo huo, katika hali ianyoonekana ni mabadiliko kwa Jeshi la Polisi katika kusimamia amani na utulivu katika maandamano na mikusanyiko ya wananchi isiyo na vurugu, leo hii hakuna bomu wala risasi iliyofyatuliwa kama ilivyozoeleka, ingawa askari walikuwa wakutosha na wamejiimarisha kwa zana zote kujihami na hatari yeyote.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO