Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

JESHI LA POLISI ARUSHA LAKAMATA NYARA MBALIMBALI ZA SERIKALI ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA TAYARI KWA KUSAFIRISHWA NJE YA NCHI

DSCN3279

JESHI la polisi mkoani Arusha,limekamata shehena kubwa ya nyara mbalimbali za serikali zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu,eneo la Matevesi Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha,zikiwa tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.

Nyara hizo ni pamoja na Ngozi za Simba,Chui na Mamba ,meno ya Tembo,vichwa vya

Nyani,Swala na Nyati,Pembe za kifaru,na zingine nyingi ambazo jeshi la polisi linaendelea kuzitambua.

Sambamba na hilo jeshi hilo limemtia mbaroni mtuhumiwa wa nyara hizo aliyetambulika kwa jina la Peter Leurence (55)mkazi Ngaramtoni ya chini,ambaye alikuwa akiwa amezihifadhi kwenye maboksi zaidi ya 20,kwenye nyumba yake iliyopo eneo hilo.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoni Arusha,Liberatus Sabas tukio la kukamatwa kwa nyara hizo limetokea jana majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo  eneo la kisongo mtaa wa mateves baada yak upata taarifa kutoka kwa raia wema.

Kamanda Sabas alisema kuwa baada ya jeshi hilo kupata taarifa za siri majira ya saa 5 asubuhi walifika eneo la tukio majira ya saa 7 mchana na kupata upinzani mkubwa kutoka kwa walinzi wa wanaolinda eneo hilo kwani waliwanyima kuwapa maelekezo ya kumpata mmiliki wa nyumba hiyo.

Hata hivyo alisema kwamba askari hao waliamua kumueka chini ya ulinzi kwa kumshurutisha mlinzi mmoja iliaweze kuwapa ushirikiano ambapo aliwapaita namba za simu na mtuhumiwa aliwaambia kuwa yupo magugu mkoani Manyara na angefika saa 12 majira ya jioni.

Taarifa zinadai kuwa baada ya mtuhumiwa kufika jitihada za kufanya upekuzi zilifanyika chini ya polisi wenye silaha za moto na walikuta shehena kubwa ya nyara za serekali zilizokuwa zimahifadhiwa kwenye ghala maalum na kufungwa kwenye mabox  teyari kusafirishwa kwenda kusikojulikana.

Alisema kuwa polisi waliamua kuweka ulinzi hadi kulipokucha na huku wakiendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo  na jeshi hilo linaendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo pamoja na watoto wake wawili waliokutwa wakiishi kwenye nyumba hiyo.

Aidha kamanda Sabas alisema kuwa kesho yake polisi waliendelea kufanya upekuzi na kubaini mabox zaidi ya 20 yenye nyara mbali mbali miongoni mwa nyara hizo alizitaja kuwa ni Ngozi za Chui.Simba,Tembo na Mamba pia kulikuwemo vichwa vya nyani,chui,swala nyati,pembe za faru ,meno ya tembo na nyingine nyingi ikiwemo mfuko wa silaha inayosadikiwa kuhifadhia silaha.

Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa alisema kuwa Watuhumiwa bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano na watafikishwa kwenye mahakama pindi upelelezi wa tukio hilo utakapo kamilika.

DSCN3284

DSCN3273

pichani; Mtuhumiwa wa nyara za serekali Peter Laurence mwenye kofia
katikati akiwa na maofisa wa jeshi la polisi chini ya ulinzi ,eneo la
kisongo mtaa wa mateves nje kidogo ya jiji la Arusha baada ya
kukamatwa na shehena ya nyara za serikali  nyumbani kwake.

DSCN3287

DSCN3290

Pichani ni ngozi ya mamba ambayo ilikutwa kwenye ghala la mtuhumiwa
ikiwa ni sehemu ya nyara mbali mbali zilizokutwa kwenye ghala hilo
ikiwemo meno ya tembo,vichwa vya simba,vichwa vya nyati,ngozi ya
simba,ngozi ya tembo na nyara nyingine nyingi za wanyama mbali
mbali.(picha zote na mahmoud ahmad  wa Jamii blog Arusha

Published by Pamela Mollel on January 7, 2013

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO