UPANDE wa mashitaka katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda (45) na Samson Mwigamba umebadilisha hati ya mashitaka.
Kutokana na mabadiliko hayo, washitakiwa hao walisomewa upya mashitaka baada ya kuongeza mshitakiwa wa tatu, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi, Theophil Makunga.
Mbali na kuongezwa kwa mshitakiwa huyo na sasa kuwa washitakiwa watatu katika kesi hiyo, upande huo sasa unawashitaki chini ya Sheria ya Magazeti iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Awali washitakiwa Kibanda na Mwigamba walikuwa wakishitakiwa chini ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Upande wa mashitaka waliomba washitakiwa Mwigamba na Kibanda kusomewa maelezo ya awali kwa sababu upelelezi umekamilika. Baada ya kuwasomewa mashitaka mapya, kesi hiyo iliahirishwa na maelezo ya awali yamepangwa kusomwa Machi 26 mwaka huu.
Kwa mujibu wa hati hiyo mpya ya mashitaka iliyosomwa Wakili wa Serikali, Beatrice Kaganda katika mashitaka ya kwanza Kibanda na Mwigamba wanadaiwa kuandika na kuchapisha habari yenye uchochezi Novemba 30 mwaka jana.
Read more...
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment