Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Bei Mpya Ya Mafuta Yatajwa..


MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza kupanda kwa bei ya mafuta kuanzia jana. Akizungumza Dar es Salaam juzi, Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo alisema bei ya bidhaa za petroli imeongezeka kunatokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaa hizo katika soko la dunia. Alieleza kuwa petroli imepanda kwa asilimia 2.55 kwa lita, dizeli imepanda kwa asilimia 0.14 wakati mafuta ya taa yamepanda kwa asilimia 1.03 katika soko hilo.

Kwa upande wa bei ya jumla, Kaguo alisema petroli itauzwa kwa Sh 1,975.64 wakati dizeli itauzwa Sh1,915.64 na mafuta ya taa Sh1,907.47.

Alisema kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei ya kikomo na kuvitaka vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

Savey ya bei mpya kwa Jiji la Arusha umeonesha kuwa kwa vituo vingi petrol sasa inauzwa kwa sh 2,228 kwa lita, diseli ikiuzwa sh 2,179 kwa lita ma mafuta ya taa sh 2,075 kwa lita.

Mbali na taarifa hiyo, Kaguo alisema pia nchi inayo akiba ya kutosha, takribani lita milioni 152 kwa aina zote ambazo zinaweza kutosheleza mahitaji kwa hadi siku 52. Mahitaji ya mafuta nchini ni lita milioni tano kwa siku. Mbali na akiba hiyo, alisema meli nane ziko bandarini moja ikiendelea kushusha mafuta ya dizeli na petroli na meli zinatarajia kumaliza kupakua mafuta mwishoni mwa mwezi huu
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO